Uhamisho wa Mzize Esperance bado

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Aug 2025
Uhamisho wa Mzize Esperance bado

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema bado klabu haijafanya maamuzi juu ya ofa walizopokea kwa ajili ya mshambuliaji Clement Mzize

Tangu wiki iliyopita kumekuwa na taarifa kuwa klabu ya Esperance ya Tunisia iko katika hatua za kukamilisha mchakato wa uhamisho wa mshambuliaji huyo aliyeitumikia Yanga kwa misimu mitatu sasa akiwa bado ana mkataba wa miaka miwili

Kamwe amekiri kuna michakato inaendelea lakini ifahamike mpaka sasa bado Mzize ni mchezaji wa Yanga

"Clement Mzize bado ana mkataba na Yanga hivyo kwa sasa ni mali yetu mashabiki ninapenda kuwahakikishia kuwa mchezaji tupo naye hajaondoka"

"Kuhusu ofa kuna ofa zaidi ya mbili kwa mchezaji wetu hizo zinafanyiwa kazi. Makubaliano yakifika taarifa itatolewa kwa kuwa mchezaji bado yupo hivyo hakuna tatizo kuhusu wengine kusema hivi na vile, viongozi tupo na masuala ya kimkataba yanatatuliwa kwa mkataba," alisema Kamwe

Mzize amezivutia timu nyingi katika dirisha hili, uhamisho wake umekumbana na sintofahamu kila mara kutokana na mvutano unaojitokeza baina ya Wasimamizi wa mchezaji huyo na Yanga

Yanga imeridhia baadhi ya ofa lakini changamoto inajitokeza upande wa wasimamizi wa mchezaji ambao nao wana ofa zao

Kwa mchezaji mwenye mkataba wa zaidi ya miezi sita, timu inayomuhitaji inapaswa kuwasiliana na timu inayommiliki kwanza ili kupata ruhusa ya kuzungumza na mchezaji ambapo kama makubaliano yanafikiwa, mchakato wa uhamisho ndio huanza

Hakuna utaratibu wa wakala kuwasilisha ofa kwa niaba ya timu inayotaka kumnunua mchezaji mwenye mkataba wa zaidi ya miezi sita

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’