Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewahamasisha Watanzania kujitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Ijumaa, August 22 katika mchezo wa robo fainali michuano ya CHAN dhidi ya Morocco
Akizungumza katika Mkutano maalum wa hamasa kuelekea mchezo huo wa kihistoria kwa Tanzania, Kamwe alisema ni jukumu la kila Mtanzania kuiunga mkono timu ya Taifa lengo likiwa kutinga nusu fainali
Kamwe ametangaza kauli mbiu maalum kuelekea mchezo huo ni HII NIMO...!
"Kuelekea mchezo huu tunakwenda na slogan ya HII NIMO, Mtanzania yeyote anayetusikiliza kama ulikosa mechi iliyopita sema HII NIMO na hakikisha unamwambia jirani yako"
"Tiketi zimeanza kuuzwa leo kwenye mitandao na vituoni tusisubiri ifike Ijumaa ndio tuanza kuzigombania"
"Tuwape ujumbe Morocco kuwa sisi tunautaka mchezo huu kwelikweli. Tumeshajaza sana huu uwanja, tuende tukaonyeshe tuko tayari"
"Naamini Watanzania kwenye hili tutashirikiana na Ijumaa tutakuja kwa wingi kuisapoti timu yetu," alisema Kamwe