Yanga itazindua na kuuza jezi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Aug 2025
Yanga itazindua na kuuza jezi

Kuelekea uzinduzi wa jezi za klabu ya Yanga 2025/26, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema baada ya uzinduzi utakaofanyika saa 6 mchana, jezi zitapatikana Makao Makuu ya klabu, Jangwani na maduka ya GSM

Kamwe ametangaza kauli mbiu maalum kuelekea tukio hilo ni TUNAZINDUA TUNAUZA. Amesema wameandaa utaratibu tofauti wa kutambulisha jezi akiwataka mashabiki kukaa karibu na kurasa rasmi za Yanga mitandao ya kijamii kujionea

"Dhumuni kubwa la kukutana nanyi ndugu wanahabari ni kuwajuza wanachama wa Yanga wote Duniani kwamba Kesho tunakwenda kuzindua Jezi zetu za ligi msimu wa 2025/26, Uzinduzi huu utafanyika kesho saa 6 mchana. Uzinduzi huu utaambatana na Kuuza jezi hizi na ndiyo maana tumekuja na Kauli ya TUNAZINDUA TUNAUZA"

"Tutakuwa na namna ya kipekee ya kuzindua mtoko wetu, hii ni namna ambayo itawashangaza, itawafurahisha na itawafikirisha kwenye kile sisi tunachokiwaza kuhusu biashara. Hivyo kaeni karibu na mitandao ya Yanga SC ili mjionee wenyewe"

“Mambo ya jezi sisi Yanga tulishavuka huko, tulishaweka Standard yetu na hivi sasa tupo kwenye mtoko wa kimataifa, daraja letu lilikuwa juu na sasa tuko juu zaidi kwenye kutengeneza mtoko mkubwa wa kimataifa, tunawaza sasa mtu akifikiria kuoa basi avae mtoko huu, mtu akiwaza kwenda Out aanze na mtoko huu,” alisema Kamwe

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
21h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’