Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ameahidi kurejea na vifaa maalum vitakavyomsaidia kupima maendelea ya wachezaji wake.
Zahera alirejea DR Congo kwa majukumu ya timu ya Taifa ambapo May 28 ataiongoza timu hiyo kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Nigeria.
Vifaa hivyo vyenye GPS vina uwezo wa kupima kasi na uwezo wa mchezaji katika kuhimili mikikimikiki kwa muda mrefu.
Katika mahojiano na gazeti la Mwanaspoti, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika amesema Zahera ameahidi kununua vifaa hivyo kwa pesa zake na atakuja navyo wiki ijayo baada ya kumaliza majukumu ya timu ya Taifa.
Nyika amesema Zahera amepania kubadilisha mambo mengi katika kikosi na anataka kujua kila mchezaji ana uwezo gani wa kukimbia na anataka kuona uwezo wa mwili wake kuwa tayari kwa mazoezi hayo na kuamua kuleta vifaa hivyo.
Amesema mara baada ya kuleta vifaa hivyo atavitumia kuangalia ubora wa wachezaji hao na watakaoonekana na uwezo mdogo wataondolewa haraka huku watakaosalia wataanza mazoezi makali ya kocha huyo.
Zoezi la kuwapima mara kwa mara litaendelea na kama watabainika wengine kushuka uwezo wanaweza kuondolewa.
“Kocha anaonyesha yuko siriazi kweli na kazi yake tulikutana naye kama kamati na akatuambia anaenda kwao, kule kuna vifaa maalumu atakavyorudi navyo, ili kutumia kuwapima wachezaji,†alisema Nyika.
“Vifaa hivyo ni maalumu kupima uwezo wa mchezaji kukimbia, pia uwezo wa mwili wake kuweza kuhimili mazoezi ambayo atakuwa anayatoa, kilichotushangaza tulitaka tumsaidie kununua lakini ametuzuia amesema atakuja navyo mwenyewe.â€

ADVERTISE HERE