Uongozi wa klabu ya Yanga leo umeendesha Semina maalum kwa Yanga Princess kuelekea msimu mpya wa mashindano 2025/26
Makamu wa Rais wa Yanga Arafati Haji aliongoza semina hiyo ambayo pia ilihudhuriwa maafisa wengine waandamizi wa Yanga akiwemo Mtendaji Mkuu, Andre Mtine
Akizungumza katika semina hiyo, Arafat alieleza kuwa na matarajio makubwa kwa kinadada hao kufanya vizuri katika ligi kuu ya Wanawake msimu ujao

Arafat alisema baada ya miaka mitatu ya kujenga kikosi, anaamini ni wakati kwa kuwania taji la ligi kuu
"Kocha wa wetu Edna Lema amesema atahakikisha anabeba ubingwa wa ligi. Najua inawezekana. Hata Roma haikujengwa kwa siku moja. Nia yetu ni kuhakikisha tunapokwenda kuongea na wanachama tuende na kombe la ligi Kuu. Tumejaribu kuboresha kikosi kwa miaka mitatu. Nina matumaini makubwa na kikosi chetu," alisema Arafat
Nae mtendaji Mkuu wa Yanga Andre Mtine amewahakikishia Yanga Princess kuwa wana sapoti ya uongozi kwa asilimia 100
Mtine amesema soka la Wanawake linapitia changamoto nyingi lakini uongozi unajitahidi kukabiliana na changamoto hizo
"Ninajivunia sana jitihada zetu. Sisi kama uongozi tupo nanyi bega kwa bega. Soka la Wanawake limepitia changamoto nyingi lakini ukweli ni kwamba tumejitahidi kwa kiwango kikubwa. Zipo changamoto za kiutamaduni lakini nyie mmekuwa mfano wa kuigwa. Msikate tamaa. Piganieni ndoto zenu," alisema




