Safu ya ushambuliaji Yanga haitakamatika msimu Ujao

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Aug 2025
Safu ya ushambuliaji Yanga haitakamatika msimu Ujao

Klabu ya Yanga imejipanga kuhakikisha msimu ujao inakuwa na safu kali zaidi ya ushambuliaji, baada ya nyota wake Clement Mzize kuthibitisha kubaki klabuni. Hatua hii imezidisha nguvu za mabingwa hao mara baada ya kumsajili Mcongomani Andy Boyeli, akiungana na Mzize pamoja na Prince Dube.

Katika mchezo wa Rayon Day dhidi ya Rayon Sports, Boyeli alionyesha thamani yake mara moja kwa kufunga bao na kutoa asisti, Yanga ikishinda 3-1. Hata kwenye kambi ya maandalizi Avic Town, Boyeli ameendelea kuonesha ubora akipambana bega kwa bega na Dube, ambaye msimu uliopita alikuwa mhimili wa safu ya ushambuliaji ya Yanga.

Mzize aliibuka mfungaji bora wa Yanga kwenye Ligi Kuu msimu uliopita akifunga mabao 14, akimaliza akiwa nyuma ya Jean Ahoua wa Simba (16 mabao). Prince Dube alifunga mabao 13 licha ya kupatwa na majeraha mwishoni mwa msimu yaliyomzuia kuongeza hesabu yake.

Kwa pamoja, washambuliaji hawa wawili walichangia mabao 27 msimu uliopita, na sasa ujio wa Boyeli unatarajiwa kuongeza makali zaidi.

Boyeli na Dube ni washambuliaji wa kati asilia, lakini Yanga ina faida kubwa zaidi kupitia Mzize, ambaye kocha Romain Folz anaweza kumtumia pia kama winga. Hii inampa nafasi ya kubadilika kulingana na mbinu, hasa ikizingatiwa kuwa timu imewaongeza pia Celestin Ecua na Offen Chikola kwa nafasi za pembeni huku Pacome Zouzoua akifanya vyema katika eneo hilo

Kwa kuangalia ubora wa washambuliaji waliopo, Yanga inakwenda kwenye msimu mpya ikiwa na safu imara ya ushambuliaji. Boyeli akiongeza nguvu mpya, Dube akiwa na kiu ya kuendeleza ufalme wake, na Mzize akionesha ukomavu, inawezekana kabisa kuona rekodi mpya za mabao zikivunjwa msimu ujao.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
1h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
1h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
5h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
23h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’