Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji leo ameongoza kikao maalum cha maandalizi kuelekea Wiki ya Mwananchi kilichofanyika Makao Makuu ya klabu ya Yanga, Jangwani jijini Dar es salaam
Kikao hicho kiliwahusisha viongozi wa Matawi, Wazee wa Yanga na Viongozi wa makundi mbalimbali ya Hamasa
Shamrashamra za Wiki ya Mwananchi zinatarajiwa kuanza Septemba 05 na kuhitimishwa Septemba 12 pale uwanja wa Benjamin Mkapa
Katika wiki ya Mwananchi, mashabiki na wanachama wa Yanga watashiriki katika matukio mbalimbali ya kijamii kama kufanya usafi mahospitalini na katika maeneo yanayowazunguuka, kuchangia damu na kutoa misaada kwa wale wenye uhitaji



ADVERTISE HERE