Kiungo wa Yanga Maxi Nzengeli amewataka Wanachama na Mashabiki wa timu hiyo kukata tiketi zao na kuhakikisha wanajitokeza kwa wiki katika kilele cha Wiki ya Wananchi Septemba 12 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Msimu huu Maxi atashiriki tukio hilo kwa mara ya tatu wengi wakikumbuka pasi yake murua kwa Kennedy Musonda aliyefunga bao pekee la ushindi dhidi ya Kaizer Chiefs katika tukio lake la kwanza
Maxi amesema anatambua thamani na ukubwa wa Wiki ya Wananchi kwa wadau wote wa klabu ya Yanga hivyo wachezaji wanajiandaa vyema ili kuhakikisha wanawapa mashabiki wao furaha wanayostahili
"Siku ya Mwananchi ni siku kubwa sana kwa klabu yetu, tunafahamu kuna matukio mengi sana siku hiyo"
"Mimi akili yangu zimewekeza kwenye mechi husika ili Wananchi wapate mechi nzuri inayoendana na hadhi ya siku hii kubwa"
"Tunaomba mfike kwa wingi uwanjani kwa mtafurahia mechi nzuri sana," alisema Maxi
Yanga tayari imethibitisha itachuana na Bandari Fc ya Kenya katika kilele cha wiki ya Mwananchi Ijumaa ya Septemba 12, 2025
Kikosi cha Yanga kinaendelea kujifua Avic Town kujiandaa na Tamasha hilo kubwa zaidi la burudani nchini