Klabu ya Yanga leo itaendesha zoezi la kuchangia damu Makao Makuu ya klabu Jangwani jijini Dar es salaam
Mashabiki na wanachama wa Yanga wametakiwa kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo
Aidha Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema zoezi hilo litafanyika nchi nzima hivyo Wananchi wafike katika vituo vya afya maeneo ya karibu kushiriki zoezi hilo
Ni katika maadhimisho ya wiki ya Mwananchi ambayo itahitimishwa siku ya Ijumaa

ADVERTISE HERE