Kiungo Thabani Kamusoko ambaye alikuwa nahodha wa kikosi cha Yanga leo amesema ukaribu wa michezo yao umechangia kwa kiasi kikubwa kufanya vibaya michezo iliyopita.
Akizungumza baada ya mchezo dhidi ya Mbao FC ambayo Yanga imeondoka ushindi wa bao 1-0, Kamusoko amesema wamekuwa wakisafiri na kucheza mfululizo hivyo kukosa mda wa kupumzika.
Kamusoko akizungumza kiswahili fasaha, amesema wao kama wachezaji wanahitaji muda wa kupumzisha miili yao lakini ugumu wa ratiba umewalazimu kucheza hivyo hivyo.
May 16 Yanga ilicheza na Rayon Sports, May 20 ikacheza na Mwadui FC, leo May 22 imecheza na Mbao FC, May 25 itacheza na Ruvu Shooting kabla ya kumaliza msimu dhidi ya Azam FC May 28.

ADVERTISE HERE