Ni siku moja imesalia kuelekea Tamasha kubwa zaidi ya burudani nchini, siku ya Mwananchi ambayo itaadhimishwa kesho Ijumaa, Septemba 12 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Kuelekea siku hiyo kubwa Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki kuhakikisha wanaitumia vyema siku ya leo kumaliza tiketi chache zilizobaki
Kamwe ametamba kuwa kesho wanakwenda kuonyesha vile matamasha makubwa yanapaswa kufanyika
Kama bado hujanunua tiketi Mwananchi wakati ni huu, fika Makao Makuu ya klabu ya Yanga kujipatia tiketi yako
Lakini pia tiketi zinapatikana kupitia mitandao ya simu na kwenye vituo vilivyoainishwa



ADVERTISE HERE