Yanga yakabidhiwa hati ya uwanja Jangwani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Sep 2025
Yanga yakabidhiwa hati ya uwanja Jangwani

Klabu ya Yanga imekabidhiwa rasmi hati ya ongezeko la kiwanja cha Jangwani, kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa klabu hiyo, huku viongozi wa timu hiyo wakimtangaza GSM kuwa mwekezaji wa uwanja huo.

Waziri wa Ardhi Deogratias Ndejembi, ndiye aliyefichua hayo alipotangaza katika Kilele cha Wiki ya Mwananchi iliyofanyika jana Kwa Mkapa ambapo amesema sasa rasmi Yanga imepata kibali cha kuongezewa eneo, ili kukamilisha moja kati ya mpango wa muda mrefu waliojiwekea.

Waziri huyo ambaye naye ni Mwananchi, amesema hati hiyo ilitakiwa kutolewa ndani ya wiki mbili, lakini hata hivyo uongozi wa Wizara ya Ardhi umekamilisha mchakato huo kwa haraka kabla ya wiki mbili zilizotangazwa katika Mkutano Mkuu wa klabu hiyo uliofanyika Jumapili iliyopita.

"Tunataka klabu kubwa kama Yanga ipate uwanja wake kwa haraka, ili kuhakikisha mashabiki ambao ni Watanzani wanapata burudani."

Mara baada ya Waziri Ndejembi kumaliza kuzungumza, Rais wa Yanga, Hersi Said, amemtangaza Gharib Said Mohammed, kama mwekezaji wa uwanja huo.

"Nataka niwatangazie rasmi baada ya kupata hati kuwa, mwekezaji wa ujenzi wa uwanja huo ni ni GSM, ambaye amekuwa na Yanga bega kwa bega,” amesema Hersi.

GSM amekuwa mfadhili wa Yanga kwa misimu minne mfululizo, huku rekodi hiyo ikienda sawa na ile ya ubingwa wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho mbali na timi kufanya vyema hata katika michuano ya kimataifa.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
6h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
11h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
11h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
15h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’