Ecua ameipania dabi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Sep 2025
Ecua ameipania dabi

Baada ya kufunga bao pekee la ushindi katika mchezo wa kilele cha Wiki ya Mwananchi dhidi ya Bandari Fc juzi, kiungo mshambuliaji wa Yanga Ecua Celestin amepania kuendeleza makali yake katika mchezo unaofuata dhidi ya Simba

Kesho Jumanne, Septemba 16, Yanga na Simba zitachuana katika mchezo wa Ngao ya Jamii ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Ecua aliyepachikwa jina la utani 'Duduwasha', amesema dhamira yake ni kuwapa furaha mashabiki wa Yanga kwa kufunga mabao kila anapopata nafasi

Ecua aliwashukuru mashabiki waliojitokeza kwa wingi katika kilele cha wiki ya Mwananchi huku akifichua alitamani kucheza kwa dakika zote 90 lakini anafahamu ilikuwa mechi ambayo kila mchezaji alistahili kucheza

"Nilitaka kumuomba kocha niendelee kuwa uwanjani, lakini niliona umuhimu wa wenzangu kucheza. Bahati nzuri nilikuwa nimefunga bao kwenye mechi yangu ya kwanza mbele ya mashabiki"

"Nataka kuendelea kufunga na sasa nataka kuendelea kufunga hata kwenye mechi ijayo ili kuendeleza furaha ya mashabiki wa Yanga ambao wameonyesha mapenzi yao kwa timu," alisema Equa

Ecua ameifungia Yanga mabao matatu katika mechi zote za kirafiki ambazo Yanga imecheza kwenye pre-season

Bila shaka kocha Romain Folz atamjumuisha katika kikosi chake kitakachoanza dhidi ya Simba hapo kesho akitarajiwa kuungana na mastaa wengine akiwemo Pacome Zouzoua

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’