Yanga imetetea Ngao ya Jamii kwa msimu wa pili mfululizo baada ya kuichapa Simba bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Sio mwingine, ni yuleyule Pacome Zouzoua aliyefunga bao la Yanga kwenye kipindi cha pili akimalizia mpira ambao awali uliokolewa na mabeki wa Simba
Mkufunzi wa Yanga Romain Folz leo hakuwa na mambo mengi akianza na kikosi kilekile kilichoshinda mabao 2-0 katika wa mwisho dhidi ya Simba msimu uliopita
Mabadiliko pekee aliyofanya ni kumtumia Aziz Andabwile katika eneo alilokuwa akicheza Khalid Aucho
Unaweza ni mechi ambayo pengine Yanga wangeweza kuimaliza mapema kwa kuzingatia nafasi walizotengeneza hasa kipindi cha kwanza
Ni kipigo cha sita mfululizo Yanga wanawazawadia watani zao na kuondoka na Ngao kwa mara nyingine
Yanga hii labda itafungwa na Mahakama tu...!