Mtihani wa Folz Yanga ni huu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Sep 2025
Mtihani wa Folz Yanga ni huu

Viongozi wa Yanga hawajawahi kuridhika na mafanikio yaliyopatikana misimu iliyopita, badala yake wameendelea kuwekeza kikamilifu kuhakikisha kikosi cha timu hiyo kinabaki na ubora wa kutetea mataji yake kila msimu

Yanga, ikiwa ndiyo klabu yenye mafanikio makubwa zaidi katika historia ya Ligi Kuu Bara kwa kushinda mara 31, msimu huu inaingia na deni kubwa: kutetea taji lake na kuendeleza utawala wake.

Majukumu hayo sasa yako mikononi mwa kocha mpya, Romain Folz, raia wa Ufaransa, aliyewasili kuchukua nafasi ya Miloud Hamdi aliyetimiza wajibu wake msimu uliopita kabla ya kuondoka. Pamoja na kuanza kazi katikati ya msimu, Hamdi alihakikisha Yanga inaendeleza makali yake na kufanikisha kutwaa ubingwa.

Historia inamwekea Folz mzigo mkubwa: Yanga imebeba ubingwa wa ligi mara nne mfululizo (2021-22, 2022-23, 2023-24 na 2024-25). Utawala huu ulisimamisha rekodi ya Simba iliyokuwa imeshinda mara nne mfululizo kabla ya kupokonywa nafasi ya kwenda kwa tano.

Makocha waliowezesha mafanikio hayo ni Nasreddine Nabi (2021-22 na 2022-23), Miguel Gamondi (2023-24) na Miloud Hamdi (2024-25).

Kwa hivyo, Folz anapokabidhiwa kijiti, anapita mulemule kwenye njia waliyoacha watangulizi wake, njia ya mataji na utawala wa ndani ya nchi. Ishara ya mwanzo ni njema kwake, kwani ameanza msimu kwa kutwaa Ngao ya Jamii baada ya kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Simba, ushindi unaoashiria kuwa anaweza kuendeleza utamaduni wa mafanikio ndani ya Jangwani.

Lakini changamoto kubwa zaidi inasalia Ligi ya Mabingwa Afrika. Folz amepewa jukumu la kuhakikisha Yanga inavuka hatua ya makundi, baada ya kushindwa kufanya hivyo msimu uliopita.

Safari hiyo inaanzia Angola, ambapo Yanga kesho Ijumaa itashuka dimbani kuvaana na Wiliete SC katika mchezo wa awali wa mchujo.

Yanga ni klabu ya makombe, na historia ya makocha waliomtangulia imemwekea Folz kiwango cha juu cha mafanikio ambayo anapaswa kuipa Yanga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’