Yanga kusaka rekodi nyingine Angola

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Sep 2025
Yanga kusaka rekodi nyingine Angola

Ni saa chache zimesalia kuelekea mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali ligi ya mabingwa barani Afrika ambapo Wananchi (Yanga) wako Angola kumenyana na Wiliete S.c

Hii itakuwa mara ya tatu Yanga kucheza dhidi ya timu kutoka Angola katika mashindano ya CAF kwani pia imewahi kucheza dhidi ya Petro Atletico (CAF CL) na Sagrada Esperanca (CAF CC)

Katika michuano hiyo, Yanga imekuwa na rekodi nzuri dhidi ya timu za Angola kwani imezitoa mara mbili. Mwaka 2007 dhidi ya Petro De Luanda kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali Yanga iliiondosha Petro Atletico kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2

Mchezo wa kwanza ugenini, Yanga ilipoteza kwa mabao 2-0, lakini nyumbani ikashinda 3-0. Ikasonga mbele kwa matokeo ya jumla 3-2.

Baada ya hapo, mwaka 2016 Yanga ikacheza dhidi ya Sagrada Esperanca katika Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya awali. Mchezo wa kwanza nyumbani Yanga ilishinda kwa mabao 2-0, ugenini ikapoteza kwa bao 1-0 lakini ikavuka kwa matokeo ya jumla 2-1.

Leo Wananchi wanawania rekodi nyingine dhidi ya timu kutoka Angola, Wiliete wakianzia mechi ya kwanza ugenini na kazi wataimaliza uwanja wa Benjamin Mkapa Septemba 27

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
19h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’