Yanga imeanza vyema kampeni ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kuichapa Wiliete S.c mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Novemba 11 huko Angola
Wananchi walitawala mchezo huo kwa sehemu pengine mambo yangekuwa mabao zaidi kwa Wiliete kama Prince Dube angetumia vyema kila nafasi aliyopata
Aziz Andabwile aliitanguliza Yanga kwenye kipindi cha kwanza akifunga bao mahiri kwa shuti kali kutoka nje ya 18
Mabao mengine mawili yalipatikana katika kipindi cha pili yakifungwa na Edmund John na Dube ambaye baada ya kosakosa nyingi akaweka kambani bao la tatu
Ni ushindi ambao unawahakikishia Yanga kuondoka na Milioni 15 za goli la Mama, huku wakijiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele hatua inayofuata



ADVERTISE HERE