Matchday; Yanga vs Pamba Jiji, NBC PL, Sept 24

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Sep 2025
Matchday; Yanga vs Pamba Jiji, NBC PL, Sept 24

Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC, Young Africans SC, leo Jumatano wanashuka dimbani kuanza kampeni yao ya kutetea taji lao kwa misimu minne mfululizo, kwa kuwakaribisha Pamba Jiji ya Mwanza katika mchezo wa kwanza wa msimu. Mechi hiyo itapigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 1:00 usiku.

Yanga, maarufu kama Wananchi, wanatazamia kuanza vyema safari ya kutafuta taji la tano mfululizo ambalo litakuwa taji lao la 32 katika historia ya Ligi Kuu. Hii pia itakuwa fursa kwa mashabiki wa Dar es Salaam kuishuhudia timu yao ikicheza mechi ya ligi kwenye uwanja wa Mkapa baada ya takribani misimu miwili.

Kocha mpya wa Yanga, Romain Folz, ataiongoza timu hiyo kwa mara ya kwanza kwenye mechi ya ligi tangu alipojiunga mwishoni mwa mwezi Julai.

Hata hivyo, tayari ameshakonga nyoyo za mashabiki baada ya kutwaa Ngao ya Jamii kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba SC na pia kuibuka na ushindi wa 3-0 ugenini dhidi ya Wiliete SC katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwa upande wa wapinzani wao, Pamba Jiji, wamekuwa jijini Dar es Salaam kwa siku kadhaa kujiandaa na mchezo huu. Jana walifanya mazoezi kwenye dimba la Mkapa gizani usiku, jambo lililoibua mjadala baada ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kueleza kuwa klabu hiyo haikutoa taarifa rasmi za kufanya mazoezi uwanjani hapo saa 1 usiku.

Mashabiki wanatarajia kuona mechi ya kuvutia, huku Yanga wakisaka mwanzo mzuri wa msimu na Pamba Jiji wakipania kuendeleza rekodi nzuri msimu baada ya kupata sare ugenini dhidi ya Namungo Fc katika mechi yao ya kwanza

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
7h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’