Huyu Folz atawafunga midomo tu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Sep 2025
Huyu Folz atawafunga midomo tu

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Romain Folz, ameanza msimu wake wa kwanza kwenye Ligi Kuu ya NBC kwa kishindo baada ya kuiongoza timu yake kushinda kwa mabao 3-0 dhidi ya Pamba Jiji kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Huo ulikuwa ni mchezo wa kwanza wa ligi msimu huu kwa Wananchi, na wakaonyesha dhamira ya kulinda taji lao.

Ushindi huu pia unakuwa wa tatu mfululizo kwa Folz katika mechi za mashindano, baada ya kuifunga Simba SC bao 1-0 kwenye Ngao ya Jamii na kupata ushindi wa 3-0 dhidi ya Wiliete SC kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Hadi sasa, kikosi cha Folz kimefunga mabao 7 bila kuruhusu goli. Ukijumlisha na mechi nne za kirafiki za maandalizi ya msimu, Folz ameshinda jumla ya mechi saba zote alizoiongoza Yanga rekodi ya ushindi wa asilimia 100.

Hata hivyo, pamoja na rekodi hiyo nzuri, mitandaoni bado kumesikika sauti za ukosoaji. Baadhi ya mashabiki wamedai kuwa Yanga inashinda lakini haichezi soka la kuvutia. Hali hii si ya kushangaza kwani mara nyingi benchi jipya la ufundi hukutana na changamoto za mwanzo wa mabadiliko ya kiufundi.

Kimbinu, Folz ameendeleza falsafa iliyokuwa imeachwa na mtangulizi wake Miloud Hamdi, huku akianza taratibu kuingiza mbinu zake. Tofauti kubwa ni namna anavyothubutu kufanya rotation ya kikosi, akitumia wachezaji tofauti katika kila mechi ili kuunda kikosi kipana.

Katika mchezo dhidi ya Pamba Jiji, Folz alianza na nyota wapya sita, hali iliyosababisha kukosekana kwa muunganiko mzuri kipindi cha kwanza. Lakini baada ya kufanya mabadiliko na kuingiza wachezaji waliokuwa sehemu ya timu kwa muda mrefu, ubora na mwendelezo wa mchezo ulionekana wazi.

Hali hii ni ya mpito. Ni wazi muda ukifika, wachezaji watakuwa wamezoeana zaidi, mifumo ya Folz itakuwa imekamilika, na Yanga itaonyesha ubora wa kiwango cha juu. Hapo ndipo wakosoaji wake watakapoanza kukosa hoja.

Kwa sasa, jambo la muhimu ni kwamba Folz anaipa Yanga matokeo sahihi na kwa soka la ushindani, ushindi daima huwa ndiyo kipimo kikubwa zaidi.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
14h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
18h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
22h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’