Folz afunguka maandalizi kuikabili Wiliete Sc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Sep 2025
Folz afunguka maandalizi kuikabili Wiliete Sc

Licha ya mechi mfululizo zinazowakabili, Kocha Mkuu wa Yanga Romain Folz amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa mkondo wa pili hatua ya awali ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Wiliete SC ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Akizungumza katika mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo, Folz amesema mkakati wake ni kushinda ili kusonga mbele raundi inayofuata katika michuano hiyo

"Tunakabiliwa na mechi mfululizo lakini lazima tuwe tayari kukabiliana na ratiba hiyo msimu mzima hivyo niseme tumejipanga vyema kuelekea mchezo wa kesho"

"Hakuna mabadiliko katika malengo yetu, tunataka kuwa na mchezo mzuri, kushinda na kuwapa furaha mashabiki wetu"

"Tulikuwa na mchezo mzuri sana Angola, tuliwanyima wapinzani wetu uhuru katika uwanja wao wa nyumbani na tukaweza kufunga mabao matatu"

"Natambua hii ni ligi ya mabingwa, Wiliete SC sio timu ndogo, walikuwa na msimu bora uliopita katika ligi ya kwao, lazima tufahamu tunakwenda kucheza dhidi ya timu ngumu," alisema Folz

Aidha Folz amesisitiza ataendelea kuwatumia wachezaji wake kwa kuzingatia mahitaji ya mechi. Amesema kwa jinsi ratiba ilivyo anawahitaji wachezaji wake wote kushirikiana akiamini upana wa kikosi chake

"Linapokuja suala la kikosi kauli yangu ni moja tu, nina kikosi kipana na ni muhimu sana, tuna mashindano mengi, lakini pia naamini kila mchezaji anayeonyesha jitihada katika uwanja wa mazoezi anastahili kupata nafasi ya kucheza"

"Lakini kama tutatumia kikosi hicho hicho kila mechi ni wazi tutapotezi matumaini ya wachezaji wengine lakini pia tuna msimu mrefu, sijui kama kocha utaweza vipi kufanya vyema kwenye kila mashindano"

"Kuna mechi nyingi zinakuja mbele yetu na kuna nyakati tutahitaji kuwa katika ubora zaidi, hivyo kuhusu kufanya 'rotation' nafikiri wakati mwingine inabidi," aliongeza Folz

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’