Je kuna ulazima Yanga kusajili kipa mpya wa kigeni?

Muungwana wa Yanga By Muungwana wa Yanga
β€’
25 May 2018
Je kuna ulazima Yanga kusajili kipa mpya wa kigeni?
Ligi Kuu ya Vodacom inamalizika Jumatatu ijayo ambapo kumalizika kwake kunapisha maandalizi ya msimu mwingine wa 2018/19.

Wakati dirisha la usajili likikaribia kufunguliwa, tayari vuguvugu lake limeanza kushika kasi kwa timu kuanza kupigana vikumbo kuwania wachezaji watakaozitumikia msimu ujao.

Yanga mabingwa msimu uliopita, wamepania kwelikweli kutengeneza kikosi cha 'maangamizi' hasa baada ya kushindwa kufikia matarajio yake msimu huu.

Tayari Yanga inawajaribu wachezaji wanne wa Kimataifa ili kujiridhisha na uwezo wao kabla ya kuwapa mikataba.

Lakini kubwa ni kwamba kuna taarifa Kocha Mwinyi Zahera huenda akafanikisha usajili wa mlinda lango wa TP Mazembe Vumi Ley Matampi aliye pia kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya DR Congo.

Mkataba wa mlinda lango huyo na Mazembe inaelezwa kuwa umemalizika na pande mbili zimeshindwa kufikia makubaliano.

Swali la msingi je Yanga bado inahitaji huduma ya mlinda lango wa Kimataifa baada ya kuwa na msimu mmoja na Youthe Rostand?

Naamini kama Vumi Ley Matampi atasajiliwa ni dhahiri itabidi imuache Rostand baada ya msimu mmoja tu.

Lakini wakati huo huo Yanga inae kipa mwenye uwezo wa hali ya juu Benno Kakolanya ambaye mkataba wake unamalizika ndani ya wiki mbili zijazo.

Kama kuna ulazima wa kubadili mlinda lango kwa nini Yanga isimpe Kakolanya mkataba mpya aweze kusaidiana na 'dogo' Ramadhani Kabwili halafu akasajiliwa mlinda lango mwingine wa ndani wa kuongeza ushindani?

Gharama za kumsajili kipa wa Kimataifa ni dhahiri zitakuwa juu ukilinganisha na kipa wa ndani.

Nakumbuka msimu uliopita Simba iliamua kuachana na mlinda lango Mghana, Daniel Agyei licha ya ubora wake na kumsajili Aishi Manula huku nafasi yake wakiongeza mchezaji mwingine wa Kimataifa.

Tujadili waungwana..
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
10h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
14h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
15h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
15h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’