Mchezo wa Yanga dhidi ya Azam FC kuchezwa usiku

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 May 2018
Mchezo wa Yanga dhidi ya Azam FC kuchezwa usiku
Mchezo wa mwisho wa Yanga katika Ligi Kuu Soka Tanzania Bara dhidi ya Azam FC utachezwa saa 2:00 usiku kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumatatu ya Mei 28, mwaka huu.

Taarifa ya Bodi ya Ligi iliyotolewa na Mtendaji Mkuu, Boniface Wambura, imesema Yanga na Azam zitacheza saa 2:00 usiku ili kutoa nafasi kwa Kituo cha Televisheni cha Azam TV chenye haki za kurusha Mbashara VPL, wakati michezo mingine yote itaanza saa 10:00 jioni.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na upinzani mkali kwani Azam na Yanga zipo katika kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya pili katika ligi huku ubingwa ukiwa tayari umechukuliwa na Simba yenye pointi 68.

Kwa sasa Azam ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 55 huku Yanga inayocheza na Tuvu Shooting kumaliza michezo ya kiporo iko nafasi ya tatu na pointi 51.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’