Yanga ilirejea mazoezini jana kuanza maandalizi kuelekea mechi mbili muhimu za kusaka tiketi ya hatua ya makundi ligi ya mabingwa dhidi ya Silver Strikers zitakazopigwa Oktoba 18 (Malawi) na Oktoba 25 (Dar)
Baada ya suluhu ya bila kufungana dhidi ya Mbeye City katika mechi ya ligi kuu ya NBC, mkufunzi wa Yanga Romain Folz alitoa mapumziko ya siku tatu ambapo jana wachezaji wote ambao hawako kwenye majukumu ya timu za Taifa, waliripoti kambini
Jana kulikuwa awamu mbili za mazoezi asubuhi na jioni ambapo muda mwingi zaidi ulitumika katika mazoezi ya kimbinu
Ni wazi Folz amesikia maoni ya Wananchi na sasa anataka mabadiliko kutoka kwa wachezaji wake
Meneja wa Yanga Walter Harrison amedokeza kuwa wiki hii wataendelea na program za mazoezi asubuhi na jioni
Yanga inawakosa wachezaji 12 ambao wako kwenye majukumu ya timu za Taifa