Wanamuwekea vikwazo Jeanine sababu wanaihofia Yanga Princess - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
7 Oct 2025
Wanamuwekea vikwazo Jeanine sababu wanaihofia Yanga Princess - Kamwe

Klabu ya Yanga kupitia kwa Meneja wa Habari na Mawasiliano Ali Kamwe, imethibitisha kupokea barua kutoka TFF ikiilekeza klabu hiyo kumfanyia vipimo mchezaji wake wa Yanga Princess Jeanine Mukandayisenga raia wa Rwanda baada ya mchezaji huyo kulalamikiwa na baadhi ya timu wakimdhania kuwa ni mvulana.

Kamwe amesema uongozi wa Yanga utakutana kupitia malalamiko hayo na kuamua nini kifanyike

"Ni kweli tumepokea barua kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguj Tanzania (TFF), barua hiyo ikieleza kwamba zipo klabu ambazo zimelalamika na kuiomba TFF kumfanyia vipimo mshambuliaji wetu wa Yanga Princess Jeanine Mukandayisenga raia wa Rwanda."

"Malalamiko hayo yamefika leo (jana) na barua hiyo imeelekeza kabisa ni daktari gani anatakiwa asimamie hilo jambo. Baada ya kupokea barua hiyo, uongozi wa Yanga utakutana kupitia jambo hilo na kuamua nini kifanyike baada ya kupata maelekezo kutoka TFF."

"Mchezaji huyu amecheza kwenye kikosi cha Yanga Princess msimu uliopita na alifanya vizuri kwenye timu yetu."

"Mwaka jana wakati hatuna timu tunajitafuta hapakuwa na maneno yoyote kuhusu Yanga Princess lakini mwaka huu wamesha chungulia na wamethibisha tumejenga timu imara ndio maana chokochoko zimeanza."

"Nimewasikia JKT Queens wametangaza wanaondoka nchini Oktoba 9, 2025 wakati siku hiyo wanatakiwa kucheza mechi dhidi ya Yanga Princess yote ni kukimbia na mizengwe tu hakuna anaetamani kukutana na Yanga Princess," alitamba Kamwe

Jeanine alitua Yanga Princess msimu uliopita akitokea klabu ya APR Queens ya Rwanda. Pia ameitumikia timu ya Taifa ya Wanawake ya Rwanda kwa zaidi ya misimu minne na hakuwahi kutiliwa mashaka ya jinsia yake

Clara Luvanga nyota wa Al Nassr ya Saudia na timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Queens) aliwahi kukumbwa na kadhia kama hiyo wakati akiitumikia Yanga Princess

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
13h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
14h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
17h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
18h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
22h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
23h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →