Oktoba 18 Yanga itakuwa Malawi katika mechi ya mkondo wa kwanza kusaka tiketi ya kufuzu hatua ya makundi ligi ya mabingwa (CAFCL) dhidi ya Silver Strikers
Hivi karibu Yanga ilizindua kampeni ya Malawi Kunaendeka ikihamasisha mashabiki kusafiri na timu nchini Malawi kuwaunga mkono Wananchi katika mchezo huo
Wananchi wa mkoa wa Mbeya na maeneo ya jirani wanaendelea kuhamasika wakijiandikisha kupitia matawi yao
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe ametamba kuwa watakwenda kulitikisa jiji la Lilongwe kama walivyofanya miaka miwili iliyopita walipocheza dhidi ya Al Merrikh nchini Rwanda
Mwaka juzi mashabiki wa Yanga waliujaza uwanja wa Pele na kuweka rekodi ya aina yake kwa timu mgeni kujaza uwanja ugenini tena nje ya nchi
Kamwe amewahamasisha mashabiki kuendelea kujiandikisha ili kuwa sehemu ya historia nyingine inayokwenda kuandikwa Malawi


