Leo timu ya Taifa ya Ivory Coast itacheza mechi ya kuwania kufuzu kombe la Dunia dhidi ya Shelisheli
Kiungo mshambuliaji wa Yanga Pacome Zouzoua ameanza katika kikosi kinachoshuka dimbani majira ya saa 10 jioni
Pacome anakwenda kuandika historia ikiwa ni mara yake ya pili kuitwatimu ya Taifa, lakini hii itakuwa mara yake ya kwanza kucheza katika mechi ya mashindano tena akianza kwenye kikosi cha kwanza
Ikumbukwe Pacome ni mchezaji pekee anayecheza Afrika aliyejumuishwa katika kikosi cha Ivory Coast, mabingwa hao wa Afcon 2023

ADVERTISE HERE