Kamwe awapa pole mashabiki baada ya kupoteza Malawi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Oct 2025
Kamwe awapa pole mashabiki baada ya kupoteza Malawi

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewashukuru Wanachama na Mashabiki wa timu hiyo waliosafiri nchini Malawi kuipa hamasa timu yao katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Silver Strikers uliopigwa uwanja wa Bingu jana

Kamwe amesema mashabiki hao wamedhihirisha ukubwa wa Yanga ukanda huu wa Afrika Mashariki kwa kuingia kwa wingi uwanja wa Bingu kuliko hata wenyeji wao Silver Strikers

Msemaji huyo wa mabingwa wa nchi amesema anafahamu maumivu waliyopata baada ya kukosa ushindi hapo jana lakini anawahakikishia watatumia vyema mechi ya marudiano ili kutinga hatua ya makundi

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Kamwe ameandika ujumbe huu;

"Jana, Mashabiki Tulifanya jukumu letu. Kwa mara ya kwanza, Wamalawi walishuhudia Timu ya ugenini ikiwa na mashabiki wengi Jukwaani kuliko timu yao ya nyumbani.

Hawajawahi kuona hili huko nyuma, sio mechi zao za ngazi ya Klabu tu, hata kwa Timu za Taifa, Jana ndio mara ya kwanza waliiona KLABU KUBWA AFRIKA MASHARIKI NA KATI ikitamba jukwaani

Bahati mbaya kwetu, Dakika 90 hazikuwa na furaha kwa upande wetu. Tulipoteza mchezo kwa goli 1-0 na tukaondoka wanyonge uwanjani.

Najua maumivu yetu yalivyokuwa baada ya mchezo.

Kwa wingi wetu uwanjani, kwa jinsi Mashabiki wetu walivyojitoa na kusafiri kwa umbali mrefu kutoka Tanzania hadi kufika Malawi, Matarajio yetu yalikuwa tupate Furaha jana.

Lakini ndio Football.

Dakika 90 za jana zimekwisha Lakini Sio kwamba FURAHA yetu kwenye CHAMPIONS LEAGUE msimu huu imekwisha. Bado tuna DAKIKA 90 nyingine nyumbani.

Malengo Yetu ni KUCHEZA GROUP STAGE

Kama kuna jambo baya zaidi kwetu, ni kuendelea kuweka vichwa vyetu chini na tukaingia kwenye mtego wa kuchambua matukio ya jana, tukakwama kwenye maandalizi ya mchezo wa nyumbani.

Tusikubali hili Wananchi. tuanze sasa Maandalizi, Mtaa kwa Mtaa, Tawi kwa Tawi kuhakikisha Tunaipeleka Timu yetu GROUP STAGE.

Tuivamie hii Mechi ya Marudiano dhidi ya Silver Strikers kikubwa zaidi.

Na jambo zuri, kwenye hizi mechi za Mtoano, Jambo muhimu zaidi ni KUVUKA GROUP STAGE na sio Matokeo ya mechi moja ya ugenini.

Huzuni yetu ya jana tuigeuze kuwa msingi mkubwa wa kutupa Morali ya kufanya COME BACK ya Kibabe Jumamosi UWANJA WA MKAPA"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
21h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’