Baada ya kumaliza mechi ya mkondo wa kwanza kuwania kufuzu hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Silver Strikers, kikosi cha Yanga leo kinatarajiwa kurejea nchini kutokea Malawi
Kikosi kinatarajiwa kuondoka Lilongwe saa 10 jioni na timu inatawasili Dar saa 2 usiku
Meneja wa Yanga Walter Harrison amesema watakuwa na mazoezi asubuhi kabla ya kukwea pipa kurejea Dar jioni
Yanga itaingia kambini siku ya kesho Jumanne kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano dhidi ya Silver Strikers ambao utapigwa Jumamosi, Oktoba 25 uwanja wa Benjamiin Mkapa
Yanga itaingia kwenye mchezo huo ikiwa tayari iko nyuma kwa bao 1-0, Wananchi wakihitaji angalau ushindi wa mabao 2-0 ili kutinga hatua ya makundi
ADVERTISE HERE