Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga Alex Ngai amesema uamuzi wa kmufuta kazi kocha Romain Folz ulikuwa wa lazima kwani timu ilianza kupoteza mwelekeo
Ngai ni miongoni mwa viongozi waandamizi wa Yanga waliosafiri Malawi kushuhudia mchezo dhidi ya Silver Strikers ambao ulimalizika kwa wenyeji kuibuka na ushindi wa bao 1-0 na kuipa Yanga kazi ya kupindua meza kwenye mchezo wa marudiano utakaofanyika uwanja wa Benjamin Mkapa mwishoni mwa wiki
Kipigo hicho kilitosha kwa uongozi wa Yanga kumfuta kazi Folz mara moja huku wakimtangaza Patrick Mabedi kuwa Kaimu Kocha Mkuu
"Tulistahili kufungwa kwasababu tulionyesha kiwango kibobu kabisa, nadhani tangu tuwe viongozi wa Yanga sijawahi ona kiwango kibovu kama mchezo uliopita," alisema Ngai
Aidha Ngai amefichua Yanga inakamilisha mchakato wa kupata kocha mpya akiwahakikishia Wananchi ujio wa kocha mwenye wasifuwa Kimataifa
"Anakuja Mwalimu mwenyewe wasifu mkubwa, Mwalimu ambaye ameshafundisha klabu kubwa barani Afrika hata Duniani kwa ujumla, Mwalimu ambaye anauwezo wa kukabiliana na presha ya klabu kubwa inapokuwa imetokea," aliongeza Ngai
Yanga inarejea leo kutoka Malawi ambapo timu itangia kambini kesho Jumanne kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa pili dhidi ya Silver Strikers