Mpaka sasa Justine Zulu hajajiunga na kambi ya Yanga hiyo ikimaanisha kuwa Yanga haina mpango na kiungo huyo.
Aidha Yanga iko kwenye mchakato wa kuziba nafasi yake.
Zulu bado ni mchezaji wa Yanga kwani mkataba wake unamalizika mwezi Novemba, naamini viongozi walishamwambia hawana mpango nae atafute timu nyingine.
Kuna taarifa wakala wa mchezaji huyo ameshaanza kulalamika kuwa mteja wake 'ametengwa' na Yanga bila taarifa.
Naamini uongozi utafuata taratibu zote za kuachana salama na kiungo huyu ili baadae asije akailetea matatizo klabu ya Yanga.
Nimefurahi msimu huu Mwalimu Lwandamina amechukua hatua ya kuwafuatilia wachezaji wa Kimataifa yeye mwenyewe.
Msimu uliopita Zulu alisajiliwa bila ya kuwa na taarifa zake za kutosha.
Ni Lwandamina pekee aliyekuwa anafahamu uwezo wake na uongozi ukamuamini akasajiliwa.
Safari hii wachezaji wa Kimataifa ambao hawafahamiki wanafanyiwa majaribio kabla ya kupewa mkataba.
Hasara itakayoingia Yanga kumlipa Zulu isingekuwepo kama mfumo unaotumika sasa ungetumika msimu uliopita.

ADVERTISE HERE