Kiungo mshambuliaji Ecua Celestin bado ana deni kubwa kwa Wananchi kwani tangu atue kwa mabingwa hao Tanzania Bara, hajaonyesha kile kilichomshawishi Rais wa Yanga Injinia Hersi Said apande ndege kumfuata Ivory Coast.
Hapa tunamzungumzia mchezaji bora wa ligi kuu ya Ivory Coast (MVP) msimu uliopita pia akiwa mchezaji tegemeo katika timu ya Taifa ya Chad ambayo ameifungia mabao mawili katika mechi mbili alizoitumikia.
Sawa, anaweza kujitetea kuwa kocha aliyepita Romain Folz hakuwa akimpa nafasi ya kutosha lakini sasa chini ya Patrick Mabedi ni wakati kwake kudhihirisha thamani yake.
Kesho Yanga inahitaji nguvu yake pamoja na nyota wengine wote katika kampeni ya kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi.
Mechi dhidi ya Silver Strikers inaweza kuamuliwa na wachezaji wa aina yake, ni mechi ambayo Yanga itahitaji kasi eneo la mbele.
Kwa Ecua hii inaweza kuwa mechi ya kujitambulisha rasmi katika soka la Tanzania