Jumamosi ni kushambulia mwanzo, mwisho..

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Oct 2025
Jumamosi ni kushambulia mwanzo, mwisho..

Kila shabiki wa Yanga ana presha na dakika 90 ngumu zijazo wakati timu hiyo ikijiandaa kwenda kukabiliana na Silver Strikers ya Malawi katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kuwania kufuzu makundi.

Wakati presha ikiwa juu kwa kila Mwanayanga, kule kambini kuna kazi ameifanya Kaimu Kocha Mkuu, Patrick Mabedi raia wa Malawi huku akifahamu ili wafuzu makundi, lazima washinde kwa angalau tofauti ya mabao 2-0 baada ya ugenini kufungwa 1-0.

Kocha Mabedi ndiye aliyekabidhiwa hatma ya Yanga kwenda hatua ya makundi ya michuano ya CAF na timu inasaka rekodi ya kufuzu kwa mara ya nne mfululizo baada ya kufanya hivyo 2022-2023 (Kombe la Shirikisho), 2023-2024 na 2024-2025 (Ligi ya Mabingwa).

Mmalawi huyo alitangazwa kuchukua nafasi ya Romain Folz, ambaye uongozi wa Yanga ulisitisha mkataba wake Oktoba 18, 2025, saa chache baada ya kikosi hicho kufungwa bao 1-0 ugenini na Silver Strikers.

Katika kuhakikisha Yanga inafuzu makundi, Mabedi ambaye amewahi kusema anawafahamu vizuri wapinzani anaokwenda kukabiliana nao, kwanza anataka ukuta wake usiruhusu bao lolote akiwaandaa mabeki na viungo kukaba kwa nguvu na kwa nidhamu.

"Hatukuwa na nidhamu nzuri sana kwenye ulinzi ndio maana tuliruhusu lile bao, nimewaambia wachezaji wasirudie makosa yale, hii ni timu kubwa (Yanga) na wao ni wachezaji wakubwa," amesema Mabedi.

"Tunatakiwa kucheza kwa nidhamu lakini wawe wakatili kutoruhusu wapinzani kujipanga na hata kukaribia lango letu, kama tutaruhusu bao tutazidi kujiweka kwenye presha."

Aidha Mabedi amesema jambo la pili anataka kuona wachezaji wakimalizia nafasi ambazo watatengeneza kwa kuwa watahitaji kushambulia kwa nguvu.

Mabedi alisema Yanga haitakiwi kukaa nyuma na anataka kila nafasi ambayo wataitengeneza iwe kama haitapatikana tena ili wapate mabao ya haraka. Katika hilo, anakiandaa kikosi chenye uwezo wa kucheza kwa kasi muda wote wa mechi.

"Tupo nyumbani tutakuwa mbele ya mashabiki wetu tunaoamini watajaa uwanja mzima, tunatakiwa kuipigania klabu yetu, hapo ni muhimu kutangulia kupata mabao ya haraka."

"Tunatakiwa kuhakikisha tunakuwa na njaa ya kumalizia nafasi ambazo tutazingeneza, mpinzani anapofanya makosa tunatakiwa kumwadhibu na sio kumfanya ajipange upya."

"Hizi ni mechi kubwa, hatutakiwi kuidharau Silver Strikers, ina kocha na wachezaji wazuri lakini Yanga inaweza kuonyesha kuwa bora zaidi kwenye mchezo huu wa nyumbani ambao utaamua hatma yetu, tunatakiwa kumaliza mechi mapema," alisema.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’