Droo ya hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa (CAFCL) na kombe la Shirikisho (CAFCC) inatarajiwa kufanyika Novemba 03 Johannesburg, Afrika Kusini.
Kwa mara ya kwanza Tanzania itakuwa na timu nne katik droo hiyo ambapo Yanga wakiwa mabingwa wa Tanzania na watani zao Simba wako ligi ya mabingwa wakati Azam Fc na Singida BS zikipenya kombe la Shirikisho.
Timu 14 tayari zimekata tiketi makundi ligi ya mabingwa ambapo Pyramids na RS Berkane zitakamilisha mechi zao za mkondo wa pili kuwania tiketi Novemba 1.
Timu ambazo zimefuzu mpaka sasa kwa ligi ya mabingwa ni Al Ahly, Mamelodi Sundowns, Esperance, TP Mazembe, Yanga, Simba, Al Hilal, Petro Atletico, AS FAR, MC Alger, Rivers United, JK Kabylie, Stade Malien, Fc Lupopo na Power Dynamos.
Yanga inatarajiwa kuwekwa Pot 2 katika droo hiyo na huenda ikawa sambamba na watani zao Simba, Al Hilal na Pyramids
