Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves jana alianza rasmi majukumu yake katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dimba la KMC Complex.
Ni siku ya kwanza kazini na amefanikiwa kuondoka na alama zote tatu katika mchezo ambao unaweza kusema bado wananchi hawajaridhika na 'performance' lakini muhimu ni alama tatu
Goncalves sasa ana kazi ya kuhakikisha anarejesha lile soka burudani ambalo Wananchi wamelishuhudia kutoka kwa timu yao katika misimu minne iliyopita





ADVERTISE HERE