Yanga ni taasisi kubwa kuliko Ngoma, kila la kheri huko aendako

Muungwana wa Yanga By Muungwana wa Yanga
β€’
27 May 2018
Yanga ni taasisi kubwa kuliko Ngoma, kila la kheri huko aendako
Kwa mtazamo wangu uongozi wa Yanga umechukua uamuzi sahihi wa kuachana na aliyekuwa mshambuliaji wake raia wa Zimbabwe, Donald Ngoma.

Mimi kama shabiki wa Yanga namtakia kila la kheri huko aendako. Lakini pia namshukuru kwa mchango wake alioutoa katika klabu yangu pendwa.

Ngoma alikuwa akiigharimu Yanga pesa nyingi lakini hakuweza kuitumikia ipasavyo msimu huu kutokana na majeraha yake 'yasiyoeleweka'.

Ndiyo! ni majeraha yasiyoeleweka kwa sababu, mwenendo wa kuumwa kwake uligubikwa na mashaka mengi.

Ni yeye mwenyewe aliyekuwa anafahamu anaumwa nini na ndiye aliyekuwa na maamuzi akatibiwe wapi.

Kuna kipindi Ngoma aliondoka Yanga kwa miezi kadhaa akieleza amekwenda kwao Zimbabwe kutibiwa kwa kuwa hakuamini tiba alizokuwa akizipata Yanga.

Ngoma hakurejea kwa wakati. Tukio lililomkasirisha sana aliyekuwa kocha Mkuu wa Yanga wakati huo George Lwandamina aliyetaka mkataba wa mchezaji huyo uvunjwe.

Baada ya uongozi wa Yanga kumuandikia barua ajieleze kwa nini asitimuliwe, akarejea na ripoti ya daktari kutoka nchini Zimbabwe ikieleza kuwa amepona lakini anahitaji mapumziko ya wiki tatu kabla ya kurejea dimban.

Hiyo ilikuwa mwanzoni wa mwezi wa kwanza mwaka huu lakini wiki tatu zilipita na mchezaji huyo hakurejea dimbani mpaka wakati huu mkataba wake ulipovunjwa.

Ngoma alikuwa na manufaa na Yanga kwenye msimu wake wa kwanza tu. Msimu uliofuata ndipo alipoanza kusumbuliwa na majeraha yake yaliyomfanya aitumikie Yanga kwa nusu msimu pekee.

Kwa wale wanaokosoa uongozi wa Yanga kwa kuamua kuachana na mshambuliaji huyo wanasahau matukio yake aliyofanya huko nyuma.

Hata aina ya uondokaji wake unadhihirisha kuwa Ngoma alikuwa ni mchezaji wa maslahi, alikuwa akiuhadaa uongozi wa Yanga kuwa anaumwa kumbe pengine haikuwa hivyo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’