Pacome kamili kuikabili KMC

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Nov 2025
Pacome kamili kuikabili KMC

Baada ya kukosekana katika mchezo uliopita wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar kutokana na changamoto ya majeruhi, kiungo mshambuliaji wa Yanga Pacome Zouzoua yuko tayari kwa mchezo dhidi ya KMC utakaopigwa uwanja wa KMC Complex hapo kesho.

Pacome alipata majeraha katika mchezo wa mkondo wa pili kuwania kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa dhidi ya Silver Strikers, mchezo ambao alipachika bao la pili na kuihakikishia Yanga tiketi ya kufuzu makundi.

Pacome ameshiriki kikamilifu mazoezi ya Yanga yanayoendelea Avic Town chini ya Kocha Mkuu Pedro Goncalves kujiandaa na mchezo huo dhidi ya KMC.

Habari njema zaidi kwa Wananchi ni kuwa Pacome atakuwa na muda zaidi wa maandalizi ya mechi za makundi ligi ya mabingwa dhidi ya AS FAR na JS Kabylie zitakazopigwa mwishoni mwa mwezi.

Ni baada ya kutojumuishwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Ivory Coast ambacho kitacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Saudi Arabia Novemba 14.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’