Nyota Yanga Princess autamani ubingwa Ligi ya Wanawake

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Nov 2025
Nyota Yanga Princess autamani ubingwa Ligi ya Wanawake

Mshambuliaji wa Yanga Princess, Jeaninne Mukandayisenga amesema kama wachezaji wana kiu ya kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake na kuandika historia kwa mara ya kwanza.

Tangu Ligi ya Wanawake ianzishwe mwaka 2017 ni timu tatu tu zimenyakua ubingwa, Mlandizi Queens walioweka historia ya kuchukua kwa mara ya kwanza huku Simba Queens na JKT Queens zikibeba mara nne kila moja.

Mukandayisenga ameweka wazi huu unaweza ukawa msimu wao bora kutokana na aina ya kikosi na morali ya kila mchezaji kuutaka ubingwa huo. Aliongeza kuwa wachezaji wamejipanga kuhakikisha wanapambana kila mechi ili kuhakikisha wanatimiza malengo ya timu msimu huu.

"Tunajua ligi ni ngumu, kila timu imejipanga lakini sisi tumeweka malengo pia tunataka ubingwa. Kila mchezaji ana morali kubwa naamini huu unaweza kuwa msimu wetu wa kipekee,” amesema Mukandayisenga

Straika huyo raia wa Rwanda amesema mbali na malengo ya timu lakini binafsi anaitamani tuzo ya kiatu cha ufungaji akiamini uwezo wa kufikisha mabao 20 ndani ya msimu upo kutokana na kuzungukwa na viungo bora wa ushambuliaji.

"Ukiangalia timu yetu imesajili nyota wenye uzoefu na wana ubora mkubwa naamini kwa kushirikiana na wenzangu ndoto yangu ya kuchukua kiatu inaweza kutimia."

Mukandayisenga alijiunga na Yanga dirisha dogo la usajili uliopita akitokea Rayon Sports ya kwao Rwanda ambako alionyesha kiwango kikubwa.

Ndani ya muda mchache aliocheza Yanga Princess alifunga mabao 12 na kuisaidia timu hiyo kumaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
14h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
18h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
22h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’