Yanga Yazindua “Yanga Soccer School” kwa Ajili ya Kuibua Vipaji vya Watoto na Vijana

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
13 Nov 2025
Yanga Yazindua “Yanga Soccer School” kwa Ajili ya Kuibua Vipaji vya Watoto na Vijana

Klabu ya Yanga leo imezindua mradi wa kuibua na kukuza vipaji utakaowahusu watoto na vijana kati ya umri wa miaka 11 na 15.

Akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi iliyofanyika Makao Makuu ya klabu ya Yanga Jangwani mapema leo, Mtendaji Mkuu wa Yanga Andre Mtine alisema mradi huo unaenda kugusa ukuaji wa soka la vijana hapa nchini.

"Leo ni siku kubwa na ya kihistoria kwa Klabu yetu. Tunakwenda kuzindua mradi wa vijana na watoto wa Yanga Soccer School. Mradi huu unaenda kugusa ukuaji wa soka la vijana hapa nchini. Tuna watoto wengi sana ambao wana ndoto za kuwa wachezaji lakini wanakosa daraja sahihi. Shule hii ya soka itajumuisha watoto wa umri wa U-11, U-13 na U-15"

“Mfumo huu wa Yanga Soccer School ni moja kati ya nyenzo imara ambazo zinatumika na vilabu vikubwa duniani. Kutokana na umuhimu wa mradi huu tumekaribisha wadau wengi mbalimbali siku ya uzinduzi na mmoja wa wageni wetu ni pamoja na Pitso Mosimame, kocha wa zamani Mamelodi Sundowns na Al Ahly,” alisema Mtine

Nae msemaji wa Yanga Ali Kamwe amesema hii ni fursa kwa watoto na vijana wengi ambao wana ndoto ya kuwa wanasoka wakubwa lakini hawakuwa na maeneo maalum ya kujifunza na kuweza kutimiza ndoto zao.

"Yanga imeamua kuanzisha soccer school kwa sababu kuna watoto wengi wana uhitaji mkubwa. Sensa inaonesha kuwa watoto kuanzia 0-13 wapo milion 20. Katika kundi hili tunafahamu wapo baadhi yao ambao wanatamani kucheza mpira."

"Wazazi wengi wamekuwa wakijaribu kutafuta maeneo ambayo watoto wao wangepata mafunzo ya soka. Yanga tukaona ni muhimu kuja na shule ya watoto ya soka," alisema

Mkurugenzi wa ufundi wa Yanga Paul Mathew amesema program hii ni daraja la kutimiza ndoto za watoto wanaotamani kuwa wanasoka.

Amesema ni fursa ya kipekee kwao kwani vijana ambao watafaulu mafunzo yao watajiunga na timu za Yanga kuanzia U-17, U-20 na baadae timu ya wakubwa au kupata nafasi ya kusajiliwa na timu nyingine.

“Yanga Soccer School ni daraja la kipekee la kutimiza ndoto za watoto wanaotamani kuwa wanasoka. Kupitia mradi huu tunaweza kupata vijana ambao baadhi yao wanaweza kujiunga na timu zetu za U-17 na U-20. Yanga Soccer School ni sehemu ambayo mtoto atapata maarifa sahihi ya soka. Tunakwenda kuanzisha mtaala maalum wa kumnoa mtoto. Yanga ni taasisi inayoheshimika. Hivyo ukimleta mtoto wako hapa utakuwa umemjengea mazingira sahihi kiusalama na kitaalum”

“Huu ni ubunifu mkubwa sana ambao utatoa fursa kwa vijana wadogo kuonesha vipaji vyao na kupata elimu sahihi ya soka. Tunakwenda kuanzisha msingi imara kutoka kwa wataalam wakubwa ili kumuandaa mtoto kufikia ndoto zake. Tuna matumaini kuwa kupitia mradi tunakwenda kuzalisha magwiji mbalimbali wa soka,” alisema Mathew

Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga Ibrahim Mohamed ameeleza utaratibu wa kujiunga na program hiyo;

“Yanga Soccer School itakuwa na ada. Ada yake itakuwa 600,000 kwa mwezi wa kwanza. Kiasi cha 50,000 kitatumika kama ada ya usajili, 150,000 kwa ajili ya vifaa na 400,000 kama ada ya mafunzo. Ukishalipa ada ya 600,000 mwezi wa kwanza, mwezi unaofuata utalipa kiasi cha Tsh 400,000. Fomu zinapatikana hapa Jangwani. Kwa mawasiliano zaidi unaweza kuwasiliana kupitia namba +255673068839. Uzinduzi rasmi utafanyika tarehe 15 novemba 2025," alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE →
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE →
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE →
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE →
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE →