Baada ya kushiriki mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi Kuwait ambao timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' ilipoteza kwa mabao 4-3, nyota wa Yanga waliokuwa kwenye majukumu Stars wamerejea kuungana wenzao katika maandalizi ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya AS FAR utakaopigwa Jumamosi, Novemba 22 katika uwanja wa New Amaan Complex.
Nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto, Dickson Job na Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' walikuwa sehemu ya wachezaji wa kikosi cha Stars kilichokuwa Misri.
Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga imethibitisha kuwa mkufunzi wa timu hiyo Pedro Gonclves ametaka kikosi chake kiwasili vusiwani Zanzibar mapema kwa ajili ya kukamilisha maandalizi ya mchezo huo ambapo mapema kesho Jumanne, Yanga itaelekea Zanzibar.
Yanga imedhamiria kuanza vyema kampeni ya kuisaka robo fainali CAFCL wakihitaji ushindi dhidi ya AS FAR.
Hakuna nafasi kwa Wananchi kupoteza alama katika uwanja wa nyumbani ili kuhakikisha wanaipata tiketi ya kufuzu robo fainali.