Yanga yatangaza viingilio mchezo dhidi ya AS FAR

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Nov 2025
Yanga yatangaza viingilio mchezo dhidi ya AS FAR

Klabu ya Yanga leo imetangaza viingilio kuelekea mchezo wa kwanza wa kundi B ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya AS FAR ambao utapigwa Jumamosi, Novemba 22 katika uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Akizungumza Makao Makuu ya klabu ya Yanga mapema leo, Meneja wa habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki wa Yanga visiwani Zanzibar kujitokeza kwa wingi kujaza dimba la Amaan kuwapa hamasa wachezaji wao ambao watakuwa wakiipambania nembo ya Yanga kuwania alama tatu muhimu.

"Tunawasihi mashabiki wetu kununua tiketi mapema ili kuhakikisha wanakuwa sehemu ya historia hii kubwa ya mchezo wa hatua ya makundi CAFCL katika uwanja wa New Amaan Complex"

"Viingilio, VIP ni Tsh 30,000/-, Wings ni Tsh 20,000/-, jukwaa la Urusi ni Tsh 10,000/-, majukwaa ya Orbit na Saa ni Tsh 5,000/-"

"Mechi ya Yanga dhidi ya FAR Rabat ndio mechi kubwa zaidi kuwahi kuchezwa katika uwanja wa New Aman Complex. Huu ndio mchezo unaozungumzwa zaidi barani Afrika kwa sasa. Usiifananishe mechi hii na mechi nyingine yoyote ambayo imewahi kucheza Aman Complex."

"Hakuna mtu anatamani kusimuliwa mchezo huu. Kila mtu anatamani kuwa New Aman Complex. Hakikisha unapata Tiketi yako mapema, zimeshaanza kuuzwa leo kwenye vituo mbalimbali na kwa njia ya mtandao."

'Kwa ambao mko Zanzibar, kadi zenu mtatumia zilezile, kama ulipoteza, kesho pale nje ya uwanja wa New Amaan Complex kadi zitakuwepo, njoo mapema nunua tiketi yako mapema usikose burudani hii kubwa Afrika,” alisema Kamwe

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’