Yanga kutua Zanzibar Jumanne

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Nov 2025
Yanga kutua Zanzibar Jumanne

Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuelekea visiwani Zanzibar kesho Jumanne kukamilisha maandalizi ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya AS FAR utakaopigwa Jumapili, Novemba 22 katika uwanja wa New Amaan Complex.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema kikosi kinatarajiwa kuondoka jjijini Dar es salaam saa 23 asubuhi.

“Yanga SC itaelekea Zanzibar hapo kesho kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya FAR Rabat. Timu itaondoka saa tatu asubuhi kwa njia ya boti."

"Baadhi ya wachezaji kama Prince Dube, Celestine Ecua, Lassine Kouma waliokuwa bado kwenye majukumu ya timu zao za taifa hawatakuwepo kwenye safari hii ya kesho Lakini tayari uongozi umeshaweka taratibu zote vizuri ili wachezaji hawa wasafiri na kuungana na timu Zanzibar moja kwa moja."

“Wachezaji waliokuwa kwenye timu ya Tanzania wamesharejea na ni sehemu ya safari ya kesho. Niwaombe Wazanzibar kujitokeza kwa wingi kuipokea timu kesho na kuwaonyesha wachezaji wetu ni kwa kiasi gani mko tayari kwa ajili ya mchezo huu mkubwa wa Kihistoria. Zinakwenda kukutana timu mbili bora Afrika kwa sasa,” alisema Kamwe

Katika hatua nyingine, Kamwe amesema siku ya Alhamisi Yanga itaanza rasmi kuuza jezi maalum zitakazotumika kuanzia hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.

“Jezi mpya za Yanga kwa ajili ya msimu wa Ligi ya Mabingwa zitazinduliwa na kuanza kuuzwa siku ya Alhamisi. Nawakumbusha kuwa jezi hizi ni maalumu kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa hivyo mzigo hautakuwa mkubwa sana, Hivyo wananchi wanapaswa kuhakikisha wanajipatia jezi zao mapema. Binafsi nimeziona hizi jezi. Jambo la uhakika na ninalisema kwa kujiamini, jezi za kimataifa za msimu ni jezi za viwango vya juu sana,” alisema Kamwe

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’