Nyota wa Yanga Ecua Celestin, Prince Dube na Lassine Kouma wameripoti visiwani Zanzibar wakiungana na wachezaji wenzao katika maandalizi ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya AS FAR utakaopigwa Jumamosi, Novemba 22 uwanja wa New Amaan Complex.
Nyota hao walichelewa kutokana na majukumu ya timu za Taifa yaliyokuwa yakiwakabili.
Nyota wengine Djigui Diarra na Duke Abuya nao walitarajiwa kuwasili leo.




ADVERTISE HERE