Yanga imefunga msimu kwa kipigo kutoka kwa Azam FC baada ya kuchapwa mabao 3-1 kwenye mchezo uliopigwa katika uwanja wa Taifa Jumatatu usiku.
Yanga iliyohitaji kushinda ili kuiondoa Azam FC kwenye nafasi ya pili ilijikuta ikiwa nyuma tu mapema kwenye dakika ya nne baada ya Yahya Zayd kuitanguliza Azam FC kwa bao safi.
Mabao mengine ya Azam FC yalipatikana kwenye kipindi cha pili kupitia kwa Shabani Iddi na Salum Abubakar wakati bao la kufutia machozi kwa upande wa Yanga lilikuwa la kujifunga Abdallah Kheri.
Azam imemaliza msimu kwenye nafasi ya pili ikiwa imefikisha alama 58 wakati Yanga 'imepambana na hali yake' kwenye nafasi ya tatu ikiwa na alama 52.

ADVERTISE HERE