Fukuza wote tuanze upya! Hiyo ndio kauli ya mashabiki wengi wa Yanga baada ya jioni ya leo kuishuhudia timu yao ikilazwa mabao 3-1 na Azam FC katika mchezo wa kumaliza msimu wa ligi kuu ya Vodacom 2017/18.
Azam FC ilitawala mchezo huo na hakika matokeo hayo hayakuwa ya kushangaza.
Ni kama wachezaji wa Yanga walikuwa wanacheza ilimradi kukamilisha ratiba hakukuwa na shauku kubwa ya kusaka ushindi kama ilivyokuwa kwa upande wa Azam FC.
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ana kazi kubwa ya kukiboresha kikosi hicho ili kiweze kufanya vizuri msimu ujao.
Sidhani kama atakuwa na muda wa kutosha kuweza kutengeneza timu imara itakayoweza kuleta ushindani kwenye michuano ya kombe la Shirikisho ambayo Yanga inaburuza mkia.

ADVERTISE HERE