Wawakilishi wanne wa Tanzania katika mashindano ya CAF msimu huu Yanga, Simba, Azam Fc na Singida BS zimekamilisha mechi zao za raundi ya kwanza hatua ya makundi huku Yanga iikiwa timu pekee iliyokusanya alama tatu.
Wananchi waliichapa AS FAR bao 1-0 katika mchezo wa ligi ya mabingwa kundi B uliopigwa uwanja wa New Amaan Complex jana.
Watani zao Simba wameangukia pua baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Petro Atletico katika uwanja wa Benjamin Mkapa.
Aidha Singida BS walikubali kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya CR Belouizdad nchini Algeria huku Azam Fc nao wakichapwa mabao 2-0 na Maniema ya DR Congo
Unaweza kusema ni Yanga pekee iliyopeperusha vyema bendera ya Tanzania katika mechi za raundi ya kwanza makundi
ADVERTISE HERE