Kabylie watangaza kuuza tiketi zote

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Nov 2025
Kabylie watangaza kuuza tiketi zote

Ijumaa Novemba 28 2025 Yanga itakuwa dimbani huko Algeria kuikabili JS Kabylie katika mchezo wa pili wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL).

Ni mchezo mwingine kutoka kundi B baada ya kukamilika mechi za raundi ya kwanza Yanga ikipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AS FAR huku Kabylie wakichapwa mabao 4-1 na Al Ahly.

Wenyeji wa mchezo huo JS Kabylie wametangaza kuuza tiketi zote siku mbili kabla ya mchezo ambao utapigwa kwenye uwanja unaochukua takribani mashabiki 50,766.

Hii inaonyesha ni kwa kiasi gani mashabiki wa timu hiyo wana shauku kubwa kuishuhudia timu yao katika uwanja wa nyumbani baada ya kufungwa mchezo uliopita.

Ni wazi hautakuwa mchezo mwepesi lakini Yanga haiwezi kutishwa na mazingira hayo kwani tayari imepata uzoefu wa kucheza katika mechi zenye presha kubwa.

Misimu miwili iliyopita hapo Algeria, Yanga ilicheza fainali ya kombe la Shirikisho (CAFCC) dhidi ya USM Algeria na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mazingira magumu.

Kikosi cha Yanga kilitua Algeria jana wakiendelea na program za mazoezi kuelekea mchezo huo.

Aidha Yanga imewahi nchini humo ili kuzoea hali ya hewa ambapo kwa sasa ni kipindi cha baridi inayofikia hadi nyuzi joto 10.

Vijana wa kocha Pedro Goncalves leo watafanya mazoezi katika viwanja vya hoteli Le Relais Vert na kesho kukamilisha maandalizi katika uwanja wa Hocine Aït Ahmed ambao mchezo huo utapigwa siku ya Ijumaa.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’