Mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons ambao kwenye ratiba ulikuwa ukionekana kupigwa Disemba 02, umepigwa kalenda na sasa Wananchi watashuka dimbani siku ya Alhamisi, Disemba 04 kuikaribisha Fountain Gate. Mchezo huo unatarajiwa kupigwa uwanja wa KMC Complex, saa 10 jioni.
Baada ya kurejea kutoka Algeria walikofanikiwa kupata suluhu ya bila kufungana dhidi ya JS Kabylie, nyota wa Yanga walipewa mapumziko na leo wanatarajiwa kurejea mazoezini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo.
Itakuwa mechi ya tatu ya ligi kwa kocha Pedro Goncalves ambaye alikishuhudia kikosi chake kikishinda mechi mbili zilizopita dhidi ya Mtibwa Sugar na KMC
Yanga imekusanya alama 10 kutoka mechi nne wakishinda tatu na kutoka sare mechi moja
ADVERTISE HERE