Chikupe athibitisha atabaki Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 May 2018
Chikupe athibitisha atabaki Yanga
Beki kitasa wa Yanga, Andrew Vincent Chikupe anatambua mkataba wake na klabu hiyo upo ukingoni na hatafanya maamuzi ya haraka katika kukimbilia ofa anazopata.

Pia amefunguka juu ya kuondoka kwa straika Donald Ngoma akisema aachwe aende zake.

Akizungumza na Mwanaspoti, Dante amesema Ngoma ni mshambuliaji mzuri ila kusepa kwake Yanga kwenda kutua Azam hakutaiathiri timu yao endapo mabosi wa Yanga watatafuta mshambuliaji mwenye makali zaidi ya Mzimbabwe huyo.

Dante aliyekosa mechi tatu za mwishoni mwa msimu uliofunga pazia jana Jumatatu kufuatia kuugua malaria, alisema anatambua endapo Ngoma atapona na kurejea uwanjani akili yake itataka kuifunga Yanga, lakini haoni kama kazi hiyo itakuwa rahisi kwake kwani wao wanajua wapi pa kumdhibiti.

Ò€œUongozi unatakiwa kutafuta mshambuliaji wa maana zaidi ya Ngoma ili azibe nafasi yake.

"Akipatikana huyo hata tukutane na timu yenye washambuliaji gani kazi yetu mabeki tutaifanya vizuri na sioni kama walikosea kilichotokea kwa Ngoma kinaweza kunitokea hata mimi, timu haiwezi kusubiri kwa muda mrefu kukosa huduma yako na huku timu haifanyi vizuri,Ò€ alisisitiza beki huyo mkali wa mipira ya juu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’