Beki wa kati wa Yanga Ibrahim Bacca leo ataendelea kukosekana katika kikosi kitakachoshuka dimbani kuikabili Fountain Gate katika mchezo wa ligi kuu ya NBC.
Bacca anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi tano huu ukiwa mchezo wa tatu anakosekana kwenye ligi.
Habari njema kwa Wananchi ni kuwa baada ya mechi ya leo, Bacca atabakisha mechi mbili tu kumaliza adhabu yake.
Nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto na Dickson Job wanatarajiwa kuongoza safu ya ulinzi katika mchezo huo ambao Yanga itakuwa ikiwania ushindi ili kuendeleza rekodi yake ya ushindi wa asilimia 100 katika uwanja wa nyumbani.
Wananchi wamekusanya alama 10 katika mechi nne wakishinda tatu na kutoka sare mchezo mmoja.
ADVERTISE HERE