Kiungo kiraka wa Yanga Duke Abuya jana aliondoka na tuzo ya nyota wa mchezo wa ligi dhidi ya Fountain Gate uliopigwa uwanja wa KMC Complex.
Abuya ambaye kwa sasa anatumika zaidi kama kiungo mkabaji, msimu huu amekuwa silaha muhimu ya Yanga katika eneo la kiungo.
Pasi yake kwa Pacome Zouzoua ndio iliyopelekea Yanga kupata bao la pili lililowahakikishia alama tatu muhimu kwa ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Fountain Gate.
Mapema tu, nyota ya Abuya imeanza kung'ara, Wananchi wanatarajia makubwa zaidi kutoka kwake..


ADVERTISE HERE